Amesema tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia
uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo.
Mafunzo yametolewa pia kwa wataalamu watakao hudumia wagonjwa
iwapo watatokea.
Vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia
wagonjwa, vimewekwa pia.
Wizara ya Afya ya Tanzania inaongeza uwezo wa kufanya uchunguzi,
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, ambao wasafiri wengi
kutoka nje huutumia.