Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Mkuu wa Chuo cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU Askofu Dr.Stephen Munga(kushoto)Makamu Mkuu wa Chuo cha SEKOMU Dr.Anneth Munga(watatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa(kulia) wakikata utepe kuzindua rasmi ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa wilayani Lushoto
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu chA Sebastian Kolowa Memorial University mabapo alifungua ukumbi wa mihadhara na kuhutubia wananchi.Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha SEKOMU Askofu Dr.Stephen Munga na kulia ni makamu wa chuo Dr.Anneth Munga
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasililiza kwa makini wanafunzi kutoka Irente school for the Blind wakati walipoimba shairi maalumu wakati wa sherehe za ufunguzi wa ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa katika chuo kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Wananchi kuhakikisha kuwa ifikapo Mwezi Novemba Mwaka huu, kila Shule ya Sekondari katika maeneo yao, ina maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi.