CALL FOR INTERVIEW
AT TANZANIA POLICE FORCE - MWANZA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza
linatangaza usaili kwa vijana waliomaliza form IV 2013 na Form six 2014
waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi kwa Mwaka 2014 kuwa tarehe
23/09/2014 hadi tarehe 26/09/2014 litafanya usaili katika ukumbi wa polisi
Mabatini kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa kumi na moja.
PAKUA ORODHA YA MAJINA
Muhimu:
(i) Mwombaji anaruhusiwa kufanya
usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe
zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi awe amejiridhisha kuwa ni
miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitashughulikia usaili
wa mtu ambaye hayupo kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili.
(ii) Mwombaji aliyeitwa kwenye
usaili aje na vyeti vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s)
& Leaving certificate(s)] na nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original
Birth certificate)]. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
(iii) Mwombaji awe na namba ya
simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..
(iv) Kila mwombaji aliyeitwa
kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi
la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.
Ni muhimu sana kwa kila mwombaji
kuzingatia muda wa kuanza usaili.
Kwa yeyote atayesoma Tangazo hili amwambie na mwenzake.