Kaburi la mmoja kati ya watu waliopoteza maisha
katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi ya Mwanza Coach na J4 katika eneo la
Sabasaba, Musoma, Mara limekutwa likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana leo
asubuhi.
Kwa mujibu wa chanzo
chetu kilichofika katika eneo la makaburi ya Musoma Basi, ndugu wa
marehemu
aliyetajwa kwa jina la Juma Sai walienda asubuhi kuangalia kaburi ikiwa ni siku
ya tatu tangu wafanye mazishi, ndipo walipokuta kaburi limefukuliwa na mbao zilizotumika
kuhifadhi mwili kwa imani ya dini ya kiislamu zikiwa zimewekwa pembeni.
“Mwili wa marehemu bado
uko ndani, watu wengi wako hapa na polisi wameimarisha hali ya usalama.
Madaktari wameshafika hapa na wanafanya uchunguzi kuona kama kuna kiungo chochote
kilichotolewa kwenye mwili wa marehemu. Inasikitisha sana.” Kimeeleza chanzo
chetu cha kuaminika.