Mwili wa marehemu Mussa ukiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakati wa kufanyiwa
postmoterm leo
Kijana
mmoja aliyejulikana kwa jina la Mussa Shija mkazi wa kata ya
Chibe katika
manispaa ya Shinyanga ameuawa kwa kupigwa kitu kizito kichwani na watu
wasiofahamika akiwa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililokuwa linafanyika
usiku wa kuamkia leo katika uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga
Akizungumza
na Malunde1 blog mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick
Mlekwa amesema uchunguzi wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana
huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani
kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mussa Athuman amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kijana huyo
aliuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana nje ya fensi la uwanja mdogo wa
Kambarage palipokuwa panafanyika tamasha la Fiesta.
Hata hivyo amesema jeshi la polisi litatoa taarifa kamili
baadaye kwani linaendelea kufanya uchunguzi