Sauti za mashabiki hao
imemfikia vyema Diamond Platinumz na amemua kujibu mashambulizi kwa kuandika ya
moyoni kuhusu mpenzi wake huyo akidai kuwa yeye mwenyewe ndiye chanzo cha
tatizo kwa kuwa ameendekeza maisha ya anasa na mashoga wanaompoteza.
“Nafikiri ningewaona kweli
mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa wasanii wenu….kama mngemshauri apunguze
mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda
ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya
kuwapa viwanda vya pombe…Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi
wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa
kufanyia kazi Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa aamue kunywa
maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza
nimuigizie mie???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie???? Ni juhudi zako
kwanza!...leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa
na moyo mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu
nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeew! Kama nimekuchagua Lamba ndimu usitapike.”