NAFASI ZA AJIRA
Jeshi la Magereza
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Jeshi la Magereza)
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA
Jeshi la Magereza Tanzania Bara
linatangaza nafasi za Mafunzo ya Awali ya Askari Magereza yatakayoendeshwa Chuo
cha Magereza Kiwira Tukuyu Mbeya. Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa kuwa na
sifa zifuatazo:-
MASHARTI YA KUAJIRIWA:
1. JINSI: Mvulana
au Msichana ambaye hajawahi kuoa
au kuolewa na asiwe na mtoto
2. URAIA: Awe
Raia wa Tanzania Bara
3. UMRI:
(a) Wahitimu wa
Shahada: Awe na umri wa kati ya miaka 18
na 28
(b) Wasio na
Shahada:
Awe na umri wa kati ya miaka 18 na 24
4. UREFU:
(a) Wavulana: Wawe na
urefu usiopungua Sentimeta 170.2 au Futi
5 na inchi 7
(b) Wasichana: Wawe na
urefu usiopungua Sentimeta 167.64 au
Futi 5 na inchi 4
5. SIFA
NYINGINEZO:
i) Awe
amehitimu Elimu yake kati ya Mwaka 2012 na 2014
ii) Awe
na Afya nzuri iliyothibitishwa na Daktari anayetambuliwa na Serikali
iii) Awe
hajawahi kushtakiwa wala kupatikana kwa kosa lolote la jinai
iv) Awe
na tabia na mwenendo mzuri
v) Awe
hajawahi kuajiriwa mahali popote Serikalini
7. ELIMU:
(a) Wenye Shahada katika
Fani au Taaluma zifuatazo:
(i) Shahada
ya Sheria (Laws)
(ii) Utekelezaji
wa Sheria (Law Enforcement)
(iii) Takwimu
(Applied Statistics)
(iv) Uchumi
na Mipango (Economic Planning)
(v) Mazingira
(Environmental Science and Management or Geography and Environment Studies)
(vi) Usanifu
Majengo (Architecture)
(vii) Ukadiriaji
Majengo (Building Economics)
(viii) Mipango
na Usimamizi Miradi (Project Planning and Management)
(ix) Uhandisi
wa Umeme (Electrical Engineering)
(x) Uhandisi
wa Mitambo ya Kilimo (Agricultural Engineering)
(xi) Tiba
ya Mifugo (Veterinary Medicine)
(xii) Misitu
(Forestry)
(xiii) Uchumi
Kilimo (Agronomy)
(xiv) Bima
(Insurance)
(xv) Uhasibu
na Usimamizi wa Vyama Ushirika (Cooperative Management and Accountancy)
(xvi) (Project
Planning and Management)
(xvii) Uhandisi
Mazingira (Environmental Engineering)
(xviii) Sayansi
ya Kompyuta (Computer Science)
(xix) Udaktari
wa Binadamu (Doctor of Medicine)
(xx) Ualimu
wa Masomo ya Sayansi kama Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati
(xxi) Ualimu
wa Masomo ya Biashara na Kifaransa (Commercial Subjects, Economics and French)
(xxii) Ukutubi
(Library and Information Studies)
(xxiii) Mahusiano
(Public Relations)
(xxiv) Biashara
na Masoko (Commerce in Marketing)
(b) WASIO NA
SHAHADA
1.1: Wenye Stashahada (Diploma) toka
katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i) Ukutubi
(Library)
(ii) Uchumi
na Mipango (Economic Planning)
(iii) Bima
(Insurance)
(iv) Uhasibu
na Usimamizi wa Vyama Ushirika (Co-operative Management and Accountancy)
(v) Mipango
na Usimamizi Miradi (Project Planning and Management)
(vi) Utabibu
(Clinical Medicine)
(vii) Uuguzi
(Nursing)
(viii) Maabara
(Laboratory Technician)
(ix) Mazoezi
ya viungo (Physiotherapy)
(x) Uandishi
wa Habari (Journalism)
(xi) Ufundi
Magari (Automobile Technician)
(xii) Ujenzi
(Civil Engineering)
(ix) Umwagiliaji
(Irrigation)
(x)
Mitambo ya Kilimo (Agro-Mechanics)
(xi) Umeme
(Electrical Engineering)
(xii) Usanifu
Majengo (Architecture)
(xiii) Ushauri
Nasaha (Counseling and Guidance)
(xiv) Uhandisi
Mitambo (Mechanical Engineering)
(xv) Sanaa
na Muziki (Fine and Performing Arts)
(xvi) Ualimu
wa masomo ya Biashara, Uchumi na Kifaransa
1.2: Wenye
Astashahada/ Cheti cha Majaribio ya Ufundi katika Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i) Uhandisi
Maji (Water Engineering)
(ii) Ujenzi
(Masonry)
(iii) Ufundi
Magari (Motor Vehicle Mechanics)
(iv) Umeme
wa Magari (Auto-Electrical Engineering)
(v) Waunganishaji
Nondo (Steel Fixing)
(vi) Useremala
(Carpentry and Joinery)
(vii) Bomba
(Plumbing and Pipe Fitting)
(viii) Rangi
(Spray and Painting)
(ix) Ushonaji
(Tailoring)
(x) Utengenezaji
Sabuni (Soap Making)
(xi) Ufumaji
(Embroidery)
(xii) Kutengeneza
viatu (Shoe-Making)
(xiii) Maabara
(Laboratory Technician)
(xiv) Uhitasi
(Secretarial Studies with Computer Knowledge)
(xv) Muziki
na Utamaduni (Performing Arts and Music)
(xvi) Uuguzi
na Ukunga (Nursing and Midwife)
(xvii) Utabibu
Usaidizi (Clinical Assistant)
ZINGATIO:
Waombaji wa nafasi hizi wahakikishe
wanazingatia masharti yote yaliyotajwa hapo juu. Upungufu au udanganyifu wowote
utakaojitokeza kwa kutotimiza masharti yaliyotajwa hapo juu utasababisha maombi
kutopokelewa na ikigundulika baada ya ajira mhusika atasitishwa mafunzo,
kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani.
8. NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wote watume maombi yao moja
kwa moja kwa:-
KAMISHNA JENERALI WA
MAGEREZA,
MAKAO MAKUU YA JESHI LA
MAGEREZA,
S.L.P 9190,
DAR ES SALAAM.
a) Barua
zote za maombi ziambatane na nakala za vyeti vyote vya elimu, ujuzi, Cheti cha
kuzaliwa mwombaji na picha ndogo ya hivi karibuni ya mwombaji (Passport size
photograph). Vyeti halisi na halali vitatakiwa kuoneshwa wakati wa usaili. Hati
za matokeo ya mitihani (Results Slip/ Statement) hazitakubaliwa isipokuwa kwa
wahitimu ambao vyeti vyao halisi havijatolewa na Vyuo husika pekee.
b) Watakaofanikiwa
kuitwa kwenye usaili watajulishwa kupitia katika Tovuti ya Jeshi la Magereza (www.magereza.go.tz), Magazeti na katika
Mbao za matangazo zilizopo kwenye Ofizi za Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Bwalo
Kuu la Maafisa wa Magereza lililopo Ukonga Dar es salaam.
c) Mwisho
wa kupokea maombi ni tarehe 15 Oktoba, 2014.