Tanzia: Mkosoaji
maarufu wa mitindo ya mavazi 'Fashion Police', Joan Rivers amefariki September
4 akiwa na umri wa miaka 81. Binti yake Melissa amethibitisha kifo chake katika
tamko alilolitoa kupitia US Weekly.
"Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo
cha mama yangu, Joan Rivers. Amepumzika kwa amani majira ya saa 7 na dakika 17
mchana akiwa amezungukwa na familia na marafiki wa karibu." Ameeleza
Melissa katika sehemu ya tamko lake. Joan Rivers ambaye pia alikuwa comedian
alizaliwa June 8,1933, Brooklyn, New York, Marekani. Na alianza kupata umaarufu
miaka ya 1960 alipoanza kuonekana kwenye vipindi vingi vya TV. Apumzike kwa
amani. Amina!