TANGAZA NA TAZAMA HABARI

FANYA BIASHARA YAKO IJULIKANE ZAIDII jivunie kua mwanafamilia wa tazama habari ! WEAPON FOUNDATION TANGAZA BIASHARA YAKO NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI TUNAKUSHUKURU KWA KUA MWANAFAMILIA WA TAZAMA HABARI

Tuesday, September 9, 2014

TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA MAGEREZA KUHUSU TAARIFA ZA UZUSHI ZINAZOZAGAA KUWA BABU SEYA NA MWANAE WAMEACHIWA HURU!

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani.
Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking (Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).
Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote
zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na
zinalenga
kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na
wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa
mujibu wa Sheria.
Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina
hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute,
kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.
Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
Sep 8, 2014