TANGAZA NA TAZAMA HABARI

FANYA BIASHARA YAKO IJULIKANE ZAIDII jivunie kua mwanafamilia wa tazama habari ! WEAPON FOUNDATION TANGAZA BIASHARA YAKO NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI TUNAKUSHUKURU KWA KUA MWANAFAMILIA WA TAZAMA HABARI

Friday, July 11, 2014

JAMATINI DODOMA: MOTO WA TEKETEZA VIBANDA 63 VYA WAJASILIAMALI


























Moto ukiwaka kwa kasi ya ajabu na kuteketeza mali za wajasiliamali wa jamatini mjini Dodoma.


























hili ni moja ya banda lililo teketea kwa moto na kila dhamani ndani yake hivyo kusababisha hasala kubwa mno kwa wajasilia mali walio jiwekeza katika biashara maeneo hayo























baadhi ya wajasilia mali wakijalibu kuokoa mali zao kutoka kwenye maduka yaliyo kumbwa na moto huo

Moto mkubwa umetokea katika eneo la Jamatini Manispaa ya Dodoma na kusababisha hasara ambayo thamani yake bado haijafahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi DAVID A. MISIME – SACP, amesema kuwa mnamo tarehe 11/07/2014 majira ya 20:40hrs katika eneo la Jamatini Mkoa wa Dodoma, kulitokea ajali ya moto ulioteketeza vibanda sitini na tatu (63) vya wajasiliamali wadogowadogo ingawa hapakuwa na madhara yoyote kwa binadamu. Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na hakuna mtu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.
Aidha Jeahi la Polisi Mkoa wa Dodoma wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kuweza kubaini chanzo cha moto huo. Kamanda wa Polisi anawapa pole waliounguliwa na vibanda na kupoteza mali zao na kusema kuwa inabidi kila mtu na mamlaka zote kuwa na mipango mizuri wanapojenga nyumba au vibanda vya biashara kuhakikisha wanaacha nafasi ya magari ya huduma kama zima moto kupita kwani katika tukio hili kilichowapa ugumu Jeshi la zimamoto na Polisi  kushindwa kuzima moto huo kwa haraka ni kutokana na waliojenga vibanda hivyo hawakuweka njia ya magari ya zima moto kuingia na kuzima moto huo. Tunaamini swala la mipango miji lingezingatiwa vibanda vingi pamoja na mali nyingi kiasi hicho hazingeteketea