Maefu wa wafuasi wa upinzani walikusanyika katika bustani ya Uhuru Park mjini Nairobi Jumatatu katika kile upinzani unasema ni kuishinikiza serikali kuhusu msitakabali wa amani na uchumi wa inchi ya Kenya.
Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga aliitisha mkutano katika bustani ya Uhuru kupinga masauala kadha yakiwemo ukosefu wa usalama na ajira, ubaguzi kwa misingi ya ukabila na kuipinga tume ya uchaguzi.
Bwana Odinga ambaye alishindwa kwenye uchaguzi wa urais mwaka uliopita anaishutumua tume ya uchaguzi kwa kuvuruga matokeo .
Uamuzi wa dakika ya mwisho wa mahakama ulitoa ruhusa ya kuendelea kwa mkutano huo. Mapema polisi waliwatupia vitoa machozi vijana waliokuwa wakirusha mawe.
Jana tangu asubuhi usalama uliimalishwa kila pande ya nchi ya Kenya huku polisi wakiwa wanazunguka huku na kule kuhakikisha usalama katika mkutano huo.