TANGAZA NA TAZAMA HABARI

FANYA BIASHARA YAKO IJULIKANE ZAIDII jivunie kua mwanafamilia wa tazama habari ! WEAPON FOUNDATION TANGAZA BIASHARA YAKO NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI TUNAKUSHUKURU KWA KUA MWANAFAMILIA WA TAZAMA HABARI

Tuesday, July 8, 2014

SINA NITAKACHO MKUMBUKA KIKWETE BAADA YA 2015 KAULI YA DR.SLAA


Akifanya mahojiano na gazeti la mwananchi ,Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema hakuna jambo lolote litakalomfanya amkumbuke Rais Jakaya Kikwete baada ya uongozi wake mwakani kuisha, akisema anachofanya sasa kiongozi huyo ni kuzindua miradi iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tatu na hakuna kipya anacho kifanya yeye kama yeye.
“Sina la kumkumbuka Kikwete,” alisema Dk Slaa katika mahojiano maalumu na gazeti la Mwananchi yaliyofanyika makao makuu ya Chadema, kabla ya kuorodhesha mlolongo wa matatizo yaliyoibuka katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne kuelezea sababu za kutomkumbuka kiongozi huyo wa nchi.

“Kipindi anaingia madarakani alikuwa na kaulimbiu yake ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya, lakini leo mmemsikia anaizungumza kauli hiyo? alihoji Dr. Slaa. Yeye mwenyewe ameikimbia, sasa unataka nimsifu kwa lipi,” alisema Dk Slaa baada ya kuulizwa kama kuna jambo ambalo linaweza kumfanya amkumbuke Rais Kikwete katika kipindi chake kinachokaribia miaka 10 akiwa Ikulu.
Wakati wa kampeni za urais za mwaka 2005, Kikwete alijinadi kwa kaulimbiu ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya sambamba na Maisha Bora kwa Kila Mtanzania na kushinda kwa kishindo na baadaye aliongeza neno ‘zaidi’ kwenye kampeni za mwaka 2010 huku akiibuka na miradi kama Kilimo Kwanza na sasa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).