Wakazi wa eneo la Kawe Mzimuni waliokuwa wakiishi
kwenye nyumba za Tanganyika Packers jana wameondolewa kwenye nyumba hizo ili
kumpisha mmiliki wa eneo hilo ambaye ni shirika la Nyumba la Taifa- NHC.
NHC imetoa kiasi cha
shilingi laki moja kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo ili wajisitiri lakini
wakazi hao waliopokea kiasi hicho cha fedha wamesema hakitoshelezi
mahitaji yao ya kuanza maisha mapya kwenye maeneo mengine
Azimio Milinga ni
mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mzimuni ambaye pia ni miongoni mwa wananchi
waliokumbwa na mkasa huo hii leo
Hata hivyo wananchi
wengine wa eneo hilo wamesema pamoja na kwamba walikuwa na taarifa ya
kuhamishwa kwenye eneo hilo, kitendo kilichofanyika jana cha wao kutakiwa
kuhama kwenye makazi yao ni cha ghafla.