Tuesday, August 5, 2014
OMMY DIMPOZI KUFANYA SHOW MBILI MAREKANI WEEKEND HII
Ndagushima hit maker Ommy Dimpoz mchana huu (Agosti 5) anakwea pipa kuelekea nchini Marekani anakotarajia kufanya show mbili weekend hii. Dimpoz amesema show ya kwanza itafanyika Ijumaa hii (Agosti 8) Houston ikifuatiwa na show ya Washington Jumamosi.
“Naelekea mchana huu (August 5) Marekani nitakuwa na show mbili pale weekend hii ambayo itakua ni Ijumaa Houston na Jumamosi itakuwa ni Washington” Dimpoz ameiambia 255 ya XXL ya Clouds FM. “Kwa show ya Ijumaa kutakuwa na after party kama tunafanya Ndagushima Night na itakuwa imekusanya watu wengi kutoka East Africa, nchi mbalimbali…pia itakuwa kama after party kwasababu kutakua na mkutano wa Mheshimiwa Rais Kikwete atakuwa anaongea na Watanzania Houston kwa hiyo akimaliza baadae watu watajijoin”. from tweeter