Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia
wataalamu
wa kada za afya kuwa bado kuna nafasi za kazi katika
Sekretarieti
za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Wataalamu wa
kada
zilizoorodheshwa hapa chini wanatakiwa kuwasilisha maombi yao ili
waweze
kupangiwa vituo vya kazi:
Madaktari
Bingwa/ Madaktari Bingwa wa Meno, Madaktari/Madaktari wa
Meno,
Mdaktari Wasaidizi/Madaktari Wasaidizi wa Meno,
Matabibu/Matabibu
wa Meno, Matabibu Wasaidizi, Mteknolojia wa Meno,
Wafamasia,
Watenolojia wa Dawa, Wateknolojia Wasaidizi wa Dawa,
Maafisa
Wateknolojia wa Maabara za Afya, Wateknolojia wa Maabara za
Afya,
Wateknolojia Wasaidizi wa Maabara za Afya, Maafisa Wauguzi,
Maafisa
Wauguzi Wasaidizi, Wauguzi, Maafisa Fiziotherapia,
Wafiziotherapia,
wateknolojia wa Macho, Wateknolojia Mionzi, Afisa Afya
Mazingira,
Afisa Afya Mazingira Msaidizi, Mhandisi wa Vifaa Tiba na
Mteknolojia
wa Vifaa Tiba.
Barua
ya maombi iambatanishwe na nakala ya cheti cha kidato cha nne,
cheti
cha taaluma na cheti cha kuzaliwa. Waombaji wa kada zenye
Mabaraza
ya Taaluma wawasilishe vyeti vya usajili au leseni.
Mwisho
wa kuwasilisha maombi tarehe 30/6/2014