TANGAZA NA TAZAMA HABARI

FANYA BIASHARA YAKO IJULIKANE ZAIDII jivunie kua mwanafamilia wa tazama habari ! WEAPON FOUNDATION TANGAZA BIASHARA YAKO NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI TUNAKUSHUKURU KWA KUA MWANAFAMILIA WA TAZAMA HABARI

Sunday, August 24, 2014

SIR JUMA NATURE ALIJISOMESHA KWA KUUZA VITUMBUA NA VYUMA CHAKAVU SOMA MAISHA YAKE HAPA


Wiki iliyopita Nature alielezea ujio wa kundi jipya la Wanaume Halisi baada ya kuvunjika kwa Kundi la Wanaume Family.

Wiki hii pamoja na mambo mengine, nguli huyo wa muziki wa kizazi kipya anaeleza jinsi alivyopata wakati mgumu kutunga mashairi na hali ya muziki ilivyo.

Anaeleza kuwa iliwachukua siku nyingi kutunga mashairi la wimbo mmoja na kwamba walifanya hivyo ili zidumu, hivyo shairi moja lilikuwa likimchukua hadi mwezi mzima kukamilisha kulitunga.
“Labda uwezo wetu ulikuwa mdogo, naona siku hizi mtu anatunga nyimbo 12 kwa siku. Mimi huwa nashangaa sana, au msanii mchanga anakwambia ana albamu nne ingawa inasikika kwa singo moja,”anasema Nature.
Anasema kuwa ugumu wa kazi hiyo ulimfanya hata augue homa kila alipomaliza kutunga nyimbo za albamu, kutokana na uchovu uliotokana na kuishughulisha akili bila kutaka kubugudhiwa. Nature anaeleza kuwa ilifikia wakati alikwenda kushinda ufukweni mwa bahari ili kukimbia marafiki ambao wangemsumbua wakati anatunga mashairi.
“Hakuna albamu niliyotunga bila kupata homa, hasa ya ‘Ugali’ ndiyo niliumwa sana, ndiyo sababu nikiona mtu ametunga nyimbo zaidi ya 10 kwa siku, namshangaa na kuona ana uwezo sana, “anasema Nature.
Nature anazungumzia utunzi wa sasa na mapokeo ya mashabiki akisema kuwa watunzi wengi hurudia ujumbe kutokana na kukosa umakini na kuiga, hivyo kutodumu na kuyeyuka mapema mioyoni mwa mashabiki.
Anafafanua kuwa wasanii wengi wa muziki kwa sasa wanaamini wakiimba singo moja watakuwa matajiri kutokana na kuwaona baadhi ya wanamuziki wamefanikiwa na wao kutamani hali hiyo, lakini matokeo yake wanaboronga.
Anaitaja changamoto wanakumbana nayo wasanii kwa sasa kuwa ni wanaojiita wadau wa muziki wa kizazi kipya kuwatumia vibaya wasanii na wanang’amua wanatumiwa, hupotezwa katika sanaa.
Anasema hali hiyo imekuwa inawaondoa kwenye soko wasanii mahiri kwa sababu watu wanaowaamini huwanyonya na kuwaacha hoi.
“Hapa nawataka wasanii wenzangu kuwa makini na watu hawa wanaojifanya wanapenda kuendeleza muziki na wasanii kwani mwishowe huwapoteza makusudi katika sanaa ili kujilinda wasionekane wabaya, “anasema.
Kuhusu kuwapo kwa studio nyingi za muziki ikiwamo ya kwake ( Halisi Recods), Nature alisema kuwa zinaleta ushindani unaozaa kazi bora.