Kutoka mbeya mbalali watu kumi wamefariki na wengine
saba kujeruhiwa baada ya ajari mbaya ya kugongana kwa magari mawili kutoke
angalia picha mbali mbali za tukio hilo jinsi lilivyo tokea huku umati wa watu
wakishuhudia na kujaribu kutoa msaada kwa wa hanga wa ajari hiyo
Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika
Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya
WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki
dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha
magari mawili.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne
asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili
T 237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba
za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema
ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya
mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake
ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia
lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua
tahadhari.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi
Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo
alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na
wanaume 4.
Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa
rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu
wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya
marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu
hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo
Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.