Rais Barack Obama wa Marekan amesema
mapigano yanayoendelea nchini Ukraine si matokeo ya kukua kwa maasi nchini humo
bali ni uchochezi wa Urusi.
Amesema waandamaji nchini Ukraine wamekuwa wakifanya
vitendo
hivyo kutokana na uchochezi wa Urusi ambapo anadai kuwa nchi hiyo inahusika
katika kuwasaidia silaha na gharama za fedha waasi hao.
Hata hivyo Rais Obama hajatoa mrejesho wa moja kwa moja kwa kile
ambacho NATO wamekiita umuhimu wa kuongeza majeshi ya Urusi nchini Ukraine.
Obama pia ameionya Urusi kwamba kwa kufanya hivyo itakuwa
gharama kubwa kwao na pia yaweza kuwasababishia hasara.