TANGAZA NA TAZAMA HABARI

FANYA BIASHARA YAKO IJULIKANE ZAIDII jivunie kua mwanafamilia wa tazama habari ! WEAPON FOUNDATION TANGAZA BIASHARA YAKO NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI TUNAKUSHUKURU KWA KUA MWANAFAMILIA WA TAZAMA HABARI

Wednesday, September 10, 2014

AJARI MTWARA: KIFARU CHA JWTZ CHAIPARAMIA NYUMBA NA KUSABABISHA VIFO!

 Ajali nyingine yatokea Mtwara na kuua wanajeshi watatu na raia mmoja baada ya kifaru kujaribu kukwepa lori la mabomba ya gesi na kuivaa nyumba iliyokuwa pembezoni. Kutoka Lindi kuna taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga kuhusu ajali iliyotokea Mtwara ambayo imehusisha gari la Jeshi la Wananchi
Tanzania(Jwtz)imeripotiwa asubuhi ya leo na shuhuda wa eneo hilo.

Msafara huo wa Wanajeshi ulikuwa ukitokea Mtwara kuelekea Nachingwea kwenye camp kubwa ya Jeshi na ajali hiyo imetokea maeneo ya Mnolela kijijini Lindi,kwa mujibu wa shuhuda ambaye ametoa taarifa hii kupitia kipindi cha Power Breakfast kutoka Clouds Fm amesema ajali hiyo imeua wanajeshi 3 na mwenye nyumba mmoja ambaye ni mwanamke alikua kalala ndani.

Madhara mengine yaliyotokana na ajali hii ni nyumba mbili kuharibika vibaya,majeruhi wa ajali hii wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa Mtwara.
Bonyeza play kumsikiliza shuhuda wa ajali hii.