Mkutano mkuu huu umetanguliwa na chaguzi za mabaraza ya CHADEMA kwa juma zima hili amabapo tayari mabaraza ya wazee,wanawake (BAWACHA) na vijana (BAVICHA) yamefanya chaguzi zake na kupata viongozi.
Mkutano mkuu huu pia umetanguliwa na vikao vikuu vya chama vya Kamati Kuu na Baraza Kuu.
Kwa namna ya kipekee pia leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Shujaa na Kamanda mpambanaji Freeman Mbowe.Anatimiza miaka 53
Tayari viwanja vya mlimani city vimejaa wajumbe wa mkutano mkuu na maelfu ya wafuasi wa chama hiki waliopambwa kwa mavazi maalum ya chama hicho 'Kombati' na wengine wakivaa fulana zenye rangi za chama za bluu bahari,nyekundu na nyeupe.Barabara zinazozunguka viwanja hivi za kuanzia Ubungo mpaka Mwenge zimepambwa na bendera za chama hiki.Huku nje ya ukumbi huu wa mlimani city kukiwa na Screen kubwa itakayoonyesha maelfu ya wafuasi walioko nje kila kitakachojiri ndani.
Mkutano huu pia unatarajiwa kuruhwa 'live' na luninga ya ITV na Radio one kuanzia saa 5 asubuhi.Inatarajiwa wageni mbalimbali wa kimataifa kutoka takribani nchi 15 duniani watahudhuria mkutano huu
Tukiamini mkutano mkuu huu unafuatiliwa karibu duniani kote tunawaahidi kuwaletea kila kitakachotokea hapa JF.
Karibuni sana...
Updates 1..
Mwenyekiti wa Taifa shujaa mpambanaji Kamanda Freeman Mbowe anaingia ukumbini hapa kwa shangwe kuu akisindikizwa na viongozi mbalimbali huku akizungukwa na vikosi vya ulinzi vya chama Red brigades.wageni mbalimbali wako hapa ukumbini.Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wako hapa wakiongozwa na viongozi wenza wa Ukawa Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia.Kwa upande wa chama Tawala kimewakilishwa na makamu Mwenyekiti Philip Mangula
Mkutano huu umeanza kwa Dua/Sala zilizoongozwa na Sheikh Rajab Katimba ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini amabye katika dua zake alimuomba Mungu CCM kipumzishwe madarakani.
Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye wengi wanamuita Rais Mtarajiwa Tanzania (kutokana na imani kubwa ya wananchi juu yake) akisaidiana na mkuu wa Itifaki Deogratius Munisi wanawatambulisha wageni mbalimbali walioalikwa kuhudhuria mkutano huu wakiwemo mabalozi kutoka nchi za China,Denmark,Ujerumani,Sudan, Ireland,Uingereza,Kenya nk..wakuu wa mashirika mbalimbali wa Kimataifa walioko hapa nchini,wawakilishi wa vyama rafiki vya ODM,CDU chama cha demokrasia Ghana.Yuko pia balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini.
Yumo pia msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi ambaye baada ya kutambulishwa alisimama na kushangiliwa sana na wajumbe.
Updates 2....
Zinafuata salaam mbalimbali za vyama rafiki zikianzia na mwakilishi wa Raila Odinga kutoka Kenya wa chama cha ODM kisha kufuatiwa na mwakilishi wa Kansela wa Ujeruman Agela Markel wa chama cha CDU.Pia anafuatia mwakilishi wa Rais mstaafu wa Bunge la Ulaya kutoka wafadhili wakuu wa CHADEMA wa KAS
Sasa inasomwa barua rasmi ya Waziri Mkuu mstaafu wa Australia ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya vyama vya kidemokrasia duniani ambavyo vinaundwa na vyama vyote vya kidemokrasia duniani.Ambapo salaam za vyama hivyo imemwaga sifa kemkem kwa chama hiki na wanaamini CHADEMA itakamata dola mwaka 2015
Anafuatia msajili wa vyama vya siasa jaji Francis Mutungi ambaye amwemwaga sifa kemkem kwa CHADEMA kwa uchaguzi wake wa kidemokrasia unaoendelea na amani iliyotawala ndani ya chama hiki.Amevitaka vyama vingie kuiga chama hiki.
Zinafuatia salaam kutoka TCD,PCCB..
Sasa wanafuata viongozi wa vyama vya siasa kutoa salaam zao.Anaanza Mwenyekiti wa NLD Emmanuel Makaidi ambaye amepongeza sana CHADEMA na kusema chama chake ni UKAWA damu damu.Anafuatia James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR ambaye naye anamwaga sifa kwa chama hiki akilaani uhuni unaofanywa na Mwenyekiti wa bunge la Katiba Samwel Sitta kuongoza ufisadi wa kuendelea na bunge la Katiba huku akifahamu ni wizi wa pesa za wananchi kwa sababu hakuna katiba mpya itakayopatikana kwa wakati huu.
Anafuatia Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula amabaye amemwakilisha Rais wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete na chama chake cha CCM ambaye anaomba watanzania wote waendelee kuwa wamoja kama Taifa.
Anafuatia Mwenyekiti wa CUF Professor Ibrahim Lipumba ambaye amezungumzia kwa kirefu kuhusu UKAWA na jinsi ulivyoanzishwa.Ameeleza kwa kirefu utayari wa CUF kuhakikisha UKAWA unashirikiana na kuingia madarakani mwaka 2014.Ameeleza kwa kirefu kuhusu uovu wa bunge la Katiba na jinsi wanavyohujumu kupatikana kwa Katiba mpya inayojali maoni ya wananchi.
Anafuatia sasa Msomi na mwanazuoni aliyebobea Dr Exzaveri Lwaitama akiwakilisha wanazuoni kote nchini.Anashangiliwa sana na wajumbe wote.Anasema UKAWA haihitaji kusajiliwa bali UKAWA ni movement ambayo iko kichwani mwa watanzania wote.Anawataka UKAWA kuzidi kusimama pamoja ili mwakani wachukue dola
Updates 3..
Anafuatia Katibu Mkuu wa chama Dr Wilbroad Slaa ambaye anatoa taarifa ya chama kwa mwaka 2009-2014.Amezungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na jinsi CCM walivyopora ushindi wa CHADEMA.Pia anaeleza kuhusu mafanikio ya CHADEMA kwa muda huu wa miaka mitano
Dr Slaa anazungumzia kuhusu mafanikio ya chama kwa program yake ya CHADEMA NI MSINGI na anasema chama kwa sasa kimeenea kote nchini kuanzia misingi,kata,majimbo,wilaya na mikoa.
Mapato ya chadema kwa miaka mitano yatokanayo na ruzuku ni Bilioni 8.4,pia misaada kutoka vyama rafiki ni milioni 623 na mapato yote yamepelekwa ofisi ya msajili.
Dr Slaa amewashukuru wafadhili wakuu wa CHADEMA waliokikopesha chama kwa takribani shilingi milioni 300.Anawataja wafadhili wakuu wa chama kuwa ni Shujaa mpambanaji Freeman Mbowe,Mbunge tajiri Philemon Ndesamburo,wabunge Suzan Lyimo na Grace Kiwelu.
Dr Slaa anataja matumizi mbalimbali ya chama kwa miaka hii mitano katika kuendeleza uwazi.Dr Slaa amesema kutokana na muda hatasoma hotuba yote kutokana na muda badala yake atagawa hotuba yake katika kijitabu alichokiandaa na kitagawanywa kwa wajumbe wote na waandishi wote wa habari.
Anakaribishwa mwasisi wa chama Mzee Edwin Mtei ambaye katika salaam zake anasema amefurahishwa sana kuona chama alichokianzisha akiwa mmoja leo hii kina maelfu kwa mamilioni ya wanachama kote nchini.
Updates 4...
Sasa anafuatia Freeman Aikael Mbowe Kamanda asiyechoka wala kuyumba kutoa hotuba rasmi ya ufunguzi.Mwenyekiti analetwa kwa mbwembwe kubwa kwa wimbo maalum wa chama huku vikosi vya ulinzi vya chama Red Brigade vikitangatanga ukumbi wote kwa mbwembwe kuu na kutoa heshima za kipekee kwa mwenyekiti.
Kamanda Mbowe ameanza kwa kuwakumbuka viongozi na wanachama wote waliouawa ama kufa kwa sababu mbalimbali.Amewapongeza wajumbe wote waliochaguliwa mikoani na kuwataka kulinda imani hiyo.Anawapongeza pia viongozi wote kote nchini na watumishi wa makao makuu ambao utumishi wao unakoma leo rasmi.
Kamanda Mbowe anawatambulisha rasmi viongozi wa mabaraza ya CHADEMA waliochaguliwa akiwemo Mwenyekiti wa Bawacha Halima Mdee na Katibu wake Grace Tendega,Viongozi wa Bavicha Pascal Patrobass na Katibu wake Julius Mwita na pia amewatambulisha viongozi wa wazee.
Kamanda Mbowe anaeleza kwa kirefu kuhusu historia ya chama.Anaeleza wapi chama kimetoka mpaka leo.Anawataja waasisi na viongozi wote wa chama kwa awamu zote na anasema katika waasisi wa chama 36 waliobaki hai mpaka sasa hawazidi 5.
Kamanda Freeman Mbowe ametuma salaam kwa mamluki na vibaraka wote waliodhani wanaweza kuvuruga CHADEMA.Anawaambia rasmi kwamba leo anamaliza muda wake wa uongozi chama kikiwa salama kabisa.Anasema kamwe hakuna mtu maarufu ndani ya CHADEMA na hakuna kibaraka yeyote atakayevumiliwa kuvuruga chama hiki.
Mbowe anasema chama kitaanza utaratibu rasmi wa kukagua utendaji wa viongozi kwa ngazi zote kote nchini na kiongozi ambaye atashindwa kutimiza malengo yanayotarajiwa atang'olewa madarakani.
Kamanda Freeman Mbowe anatoa sasa rasmi kauli ya chama kuhusu Uhuni na Ubatili wa bunge la katiba unaoendelea huko Dodoma.Mbowe anasema kinachoendelea Dodoma ni wizi,ubadhirifu na utapeli wa mali za umma.Anamlaani Samwel Sitta anayejifanya ndiye Rais wa nchi hii na kutapanya pesa za nchi hii kwa kadiri apendavyo bila kunyooshewa kidole na yeyote.
Mwenyekiti Mbowe ameutaka mkutano mkuu uazimie rasmi bunge batili la Katiba livunjwe mara moja.Endapo kama hilo halitafanyika uitishwe mgomo wa kitaifa kwa sekta zote na maandamano kote nchini yasiyokoma.Wajumbe wote wanasimama na kushangilia kwa shangwe kuu kuunga mkono tamko na kauli hiyo kama maazimio.
Pia Mkutano mkuu huu umeazimia wanasheria wote waangalie namna ya kufungua mashtaka kote nchini kupinga mchakato huu haramu kule Dodoma.
Mkutano mkuu pia umeazimia viongozi wote wa chama majimboni waende waandae taratibu za namna ya kushiriki migomo na maanadamano kupinga bunge haramu la Katiba.
Pia chama kikae na wenzetu wa UKAWA kukubaliana namna nyingine za kupambana na wizi na ubadhirifu unaoendelea Dodoma.
Kamanda Freeman Mbowe anawashukuru wajumbe wote wa mkutano mkuu na kutangaza rasmi kuvunja uongozi wote wa kitaifa uliokuwepo kutokana na kumaliza muda wake kikatiba.
Asanteni sana..