Msanii wa miondoko ya Bongo Bolingo Flava, H Baba
anaweza kuwa msanii wa kwanza mkubwa Tanzania kujitokeza hadharani kutaja
kiwango kidogo zaidi alichotumia kushuti video ya wimbo wake.
Bila kung’ata neno wala
kuongeza sifuri, H Baba akiwa kwenye kipindi cha
The Jump Off cha 100.5 Times Fm alieleza kuwa video ya wimbo wake mpya Tubebane aliofanya na muongozaji kutoka Mwanza ‘Saimaco’ ilimgarimu kiasi cha fedha za Kitanzania 150,000 tu.
The Jump Off cha 100.5 Times Fm alieleza kuwa video ya wimbo wake mpya Tubebane aliofanya na muongozaji kutoka Mwanza ‘Saimaco’ ilimgarimu kiasi cha fedha za Kitanzania 150,000 tu.
“Unajua watu wengi
wanaweza kukwambia ‘H Baba hatumuoni…’ waangalie video yangu niliyoshuti kwa
150,000 tu. Haina sifuri mbele. Ni laki na nusu na video inaitwa Tubebane. Ni
bonge la video…”Alisema H Baba.
“Unajua sisi wasanii
tusipende kuongea uongo kwa sababu uongo unaweza kutuletea matatizo. Matatizo
ni yapi, mashabiki wanajua sisi tuna pesa kumbe pesa hatuna.”