Mabasi yote yanafanya safari kutoka Dodoma kwenda Iringa
(upendo) na Super Feo (Songea) .
Taarifa za kutoka eneo la tukio zinasema kuwa chanzo cha
ajali hiyo ni punda aliyekatisha barabarani na mwendo kasi wa basi la
upendo bila umakini wa dereva wa basi hilo.
Abiria waliokuwa katika basi la upendo walisema kuwa
walikuwa wakilifuata basi la Super feo kwa kasi bila kuacha safety
distance (nafasi ya usalama kati ya basi moja na lingine nyuma au mbele ) hali
iliyopelekea ajali hiyo kutokea pale dereva wa basi la Super feo aliposimama
ghafla kuepuka kugonga punda aliyekuwa akikatisha barabarani.
Taarifa zinaendelea kudai kuwa dereva wa basi
la upendo amevunjika miguu na wengine wamejeruhiwa vibaya!