Katika hali ya kushangaza na iliyowaacha vinywa wazi wananchi, askari wa
kutuliza ghasia F.F.U wamesimamia zoezi la kubomoa kituo cha polisi cha wilaya
pamoja na nyumba wanazoishi askari polisi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera
kupisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 59.1 toka Kyaka wilayani Missenyi
hadi Bugene wilayani Karagwe kwa kiwango cha lami.
Ni tukio lililovuta umakini wa watu wengi huku minong'ono ikitawala ya
ukosoaji wa kauli ya polisi "Utii wa sheria bila shuruti", wakihoji
maana yake kwani nao (polisi) wamekaidi kutii sheria hadi kuletewa F.F.U
kuwashughulikia endapo wangejaribu kuleta fujo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera
(RPC) Henry Mwaibambe alipopigiwa simu juu ya tatizo hilo, simu yake imeita
bila kupokelewa.
Sisi TANROADS tunaonesha mipaka ya
barabara na polisi wanabomoa nyumba zao na kituo chao hivyo waulize wao kwanini
ubomoaji unafanywa chini ya ulinzi mkali amesema.
Hata hivyo zoezi hilo limeingiwa na
dosari baada ya kundi la nyuki kutokea na kuwashambulia wabomoaji, maaskari na
mashuhuda wa tukio hilo huku dereva akilazimishwa na wachina kuendelea na
ubomoaji licha ya kung'atwa na nyuki hao.
Ni tukio linaloshangaza na kuitia doa serikali kwa
jeshi la polisi lenye dhamana ya kulinda usalama na raia ambalo daima huhubiria
raia utii wa sheria bila shuruti sasa linaenda kinyume hadi kuletewa F.F.U
kulisimamia.
Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya Karagwe hakupatikana
kuzungumzia sakata hilo ambapo inadaiwa kuwa bomoabomoa hiyo itaigharimu
halmashauri hiyo baadhi ya ofisi zitakazobomolewa ikiwemo ofisi za wabunge wa
majimbo ya Karagwe na Kyerwa.