Sumbawanga. Maiti sita kati ya nane za watu waliofia Ziwa Tanganyika baada ya boti mbili kugongana Julai 7 wilayani Nkasi mkoani Rukwa zimepatikana.Katibu Tawala wa wilaya Nkasi, Festo Chonya alisema kutokana na miili kuharibika, serikali imetenga eneo maalumu katika kijiji cha Korongwe ambapo miili yote iliyopatikana imezikwa.Aliwata waliopatikana hadi hivi sasa kuwa ni Fatuma Masud (46) mkazi wa Mwanza ambaye alikuwa ni
Wengine ni Anastazia Alex (7) wa Korongwe, Emmanuel Manyika (28) mkazi wa Mpege na Beneth Kasomo (54) wa mkazi wa Challa na kuwa jitihada za kuitafuta miili ya watu wawili waliokufa katika ajali hiyo inaendelea. Chonya alifafanua kuwa ajali hiyo ilitokea usiku wa tarehe 7 mwezi huu saa 3 usiku ambapo boti ya abiria iliyokuwa imetokea katika Kata ya Kirando walipogongana na boti la wavuvi iliyosababisha boti la abiria kupasuka na kuzama na kusababisha vifo hivyo vya watu wanane.
source Mwananchi
source Mwananchi