Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid
Benz’, anadaiwa kukwaa kisanga kingine kibaya baada ya kukurupuka kutoka
nyumbani kwake na kwenda kumvamia staa mwenzake, Rehema Chalamila ‘Ray C’
nyumbani kwake anapoishi na kumtwanga makonde ikiwa ni siku chache tangu jamaa
huyo apate msala mwigine wa aina hiyo
Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi
iliyopita nyumbani kwa Ray C, Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo
ilisemekana kwamba Chid Benz alimvamia mishale ya saa 4:00 usiku kwa gia ya
kumsaka mzazi mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Mariam.
Ilidaiwa kwamba Chid Benz alisema kuwa alizungumza na
mpenziye huyo kwamba alitaka kwenda kumuona mwanaye ambapo Mariam alimjibu
kwamba kwa muda huo alikuwa nyumbani kwa Ray C Changanyikeni.
Huwezi kuamini baada
ya muda kama wa saa moja, Ray C na Mariam wakiwa ndani wakitazama TV, ghafla
mlango ulisukumwa kwa nguvu kisha akaingia Chid Benz na kumdaka Mariam na
kuanza kumshushia kipigo.“Yaani huo mshtuko walioupata walidhani wamevamiwa na
Al-Shabaabo
alifanikiwa kumkuta mariam na kumpa kichapo cha nguvu na baadaye mariam alipata upenyo na kukimbia ndipi chid alipo mgeukia Ray c nakumpa kipigo pia
Ray C alisema baada ya tukio hilo
alikwenda kuripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na
kufunguliwa jalada la kesi ambapo Chid Benz anasakwa na polisi.
huyu ni mwanadada Mwanaisha aliye pigwa na Chid benzi siku za karibuni ambaye kesi yake ipo mahakamani Chid Benz anadaiwa kuwa ni tatizo kwani
tukio hilo la Ray C amelifanya wakati akiwa na tukio la pili kwa wanawake kwani
kwenye Mahakama ya Mwanzo, Ilala ana kesi mbichi aliyoshitakiwa kwa kosa la
kumpiga mrembo aitwaye Mwanaisha.