Waziri wa Afya wa taifa
hilo, Aaron Motsoaledi,amesema kwamba marufuku hiyo haiwahusu raia wa nchi hiyo
ingawa watalazimika kukaguliwa kitabibu ili kubaini endapo watakuwa wamepata
uambukizo.
Nao Umoja wa Africa
umesema kwamba utaunda timu madhubuti ambayo ni maalumu kwa nchi hizo nne
kutoka Africa Magharibi zilizoathiriwa na ugonjwa huo.timu hiyo itahusisha
watabibu watakao shirikiana na watabibu wa nchi husika katika kuutokomeza
ugonjwa huu.
Pengine haya ni matunda
ya ukosoaji wa madaktari wasio na mipaka kuukosoa umoja huo wa mataifa kwa
kushindwa kuwajibika kuhusiana na ugonjwa huo.