Jaji Alvin Hellerstein
alisema toleo la wimbo “Loca” la lugha ya kihispania 2010 lilikiuka haki za
umiliki za wimbo wa mwimbaji Ramon Arias Vazquez.
Toleo la Ramon la “Loca” kwa lugha ya kiingereza-
lililotumika katika Dizzee Rascal – “halikutolewa kama ushahidi,” katika
kusikizwa kwa kesi hiyo.
Hakuna toleo lolote kati
ya matoleo hayo mawili lililotolewa Uingereza.
Hata hivyo, toleo la
kihispania – linalomshirikisha Eduard Edwin Bello Pou, anayefahamika kama El
Cata – lilitolewa na kuvuma kote ulimwenguni na kuuza zaidi ya kanda milioni
tano na kuongoza kwenye chati za kilatino kwenye Billboard Magazine.
Aidha, wimbo huo
ulikuwemo kwenye albamu yake ya 2010 ‘Sale el Sol’ iliyouzwa kwa wasikilizaji
wa Kiingereza na mada ya “The Sun Comes Out,” na matoleo yote mawili ya wimbo
huo yalikuwemo.
Katika uamuzi
uliotolewa Jumanne, jaji Hellerstein alisema kuwa, japo wimbo huo ulikuwa
umetungwa ukifuata wimbo uliokuwa umerekodiwa hapo awali na Bello [El Cata],
pia ulikuwa umenakiliwa kutoka kwa wimbo mwingine wa Arias Vasquez.
"Hakuna shaka kuwa
toleo la Shakira la wimbo huo lilitungwa likifuata toleo la hapo awali la
Bello,” jaji huyo aliandika kwenye uamuzi wake.
"Kwa hiyo,
nimepata kuwa, kwa kuwa Bello alinakili Arias, yeyote aliyeandika toleo la
Shakira pia alinaliki kwa njia isiyo ya moja kwa moja Arias,” alikata kauli.
Ramon Arias Vazquez
alitunga wimbo Loca con su Tiguere miaka ya 1990, lakini Bello amekana
kuunakili wimbo huo.
Uamuzi unatarajiwa
kuelekeza fidia atakayolipwa mlalamikaji Mayimba Music, mmiliki wa haki miliki
za hati ya Aria.
Sony ilisambaza matoleo
yote mawili ya wimbo wa Shakira, toleo la Kiingereza, na la Kihispania, lakini
tuhuma zilizotolewa ziliangazia toleo la kihispania.
Tarehe 13 Julai,
Shakira, mwimbaji wa Colombia, alitumbuiza umati na wimbo huo katika sherehe ya
kuhitimisha kombe la Dunia huko Rio de Janeiro.