Kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili iliyopita baada ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kucheleweshwa kupanda stejini kwenye Ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart, Ujerumani,
mwanamuziki huyo anadaiwa kupigwa marufuku kutia maguu nchini
humo. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini mjini humo, ambacho pia kilikuwepo
ukumbini wakati vurugu zilipoibuka, uchunguzi wa awali umeonesha kwamba gharama
ya vitu vilivyoharibiwa inakadiriwa kuwa zaidi ya Euro 128,322 sawa n ash,
milioni 280. Angalia picha zaidi jinsi watu na tukio zima lilivyo tokea